SUNGURA MJANJA NA SIMBA MKATILI

 

Na,Emakulata Msafiri

Palikuwa na msitu mkubwa uliokuwa na wanyama wengi. Msituni humo aliishi Simba, mfalme wa msitu, lakini alikuwa mkatili sana. Kila siku alitaka mnyama mmoja awe kafara ili aweze kumla. Wanyama walihofu sana.

Siku moja ikafika zamu ya Sungura. Wanyama wengine walimwonea huruma, lakini Sungura akawaambia, “Msinione mdogo, nina mpango.”

Sungura akaenda kwa Simba akiwa amechelewa sana. Simba alikasirika:
"Mbona umechelewa?" Simba akauliza kwa hasira.
Sungura akasema, “Samahani sana mfalme. Tulikuja wawili, mimi na sungura mwingine, lakini njiani tukakutana na simba mwingine aliyesema yeye ndiye mfalme wa msitu. Akanikamata na akamtia mateka mwenzangu!”


Simba alichukia sana: “Simba mwingine? Katika msitu wangu?”

Sungura akasema, “Ndiyo. Anajificha kwenye pango kubwa lenye kisima. Twende nikuonyeshe!”

Wakaenda hadi kwenye kisima kilichokuwa ndani ya pango. Simba alipoinama kutazama ndani, akaona sura yake mwenyewe ikireflekta kwenye maji. Akadhani ni simba mwingine.

Kwa hasira, Simba akarukia ndani ya kisima ili apigane na “simba mwingine” — lakini akaanguka ndani na kuzama.

Wanyama wote wakashangilia. Tangu siku hiyo, Sungura aliheshimiwa sana kwa ujanja wake.


 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments