Na, Emakulata Msafiri
Hapo zamani za kale, kulikuwa na mbuzi mweupe aitwaye Madoa. Madoa aliishi kijijini karibu na mlima. Kila siku alichunga karibu na kijito kidogo, lakini majani yalikuwa yamekauka na hakukuwa na chakula cha kutosha.
Siku moja aliona upande wa pili wa kijito kuna majani mabichi mengi. Lakini kulikuwa na daraja la kuni ambalo lilikuwa dhaifu na chini yake palikuwa na maji mengi. Madoa alitaka kuvuka, lakini wanyama wengine walimwambia, “Usithubutu! Utateleza na kuanguka!”
Lakini Madoa alikuwa jasiri. Alisema, “Nitavuka polepole na kwa uangalifu.” Alianza kuweka miguu yake kwa makini juu ya daraja. Alipofika katikati, daraja lilianza kusikika kriiik..., lakini hakutishika. Aliendelea hatua kwa hatua hadi alivuka salama.
Alipofika upande wa pili, alikula majani mabichi kwa furaha. Lakini hakuwasahau wenzake. Alirudi tena darajani (kwa uangalifu uleule), akaleta matawi na majani kwa wenzake.
Wanyama walimshangilia Madoa na wakasema, “Umetufundisha kuwa jasiri na pia kuwa mwenye moyo wa kushiriki!”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment