MAMA WA HEKIMA NA MTOTO MPUMBAVU

 


Na, Emakulata Msafiri 

Aliishi mama mmoja mjane aliyekuwa na mtoto wake mmoja wa kiume aitwaye Juma. Juma alikuwa mvivu na mjinga. Alipopata chakula, alikula peke yake bila kumshirikisha mama yake. Alipopewa kazi, hakuiifanya ipasavyo. Mara nyingi alidanganywa hata na watoto wadogo kuliko yeye.

Siku moja mama yake alimwambia, “Juma, nenda sokoni, uuze maziwa haya. Ukipata pesa, zinunue mahitaji ya nyumbani.” Mama alimpa chupa tatu za maziwa.

Juma alikwenda sokoni, lakini njiani akakutana na kijana mmoja aliyemwambia, “Nikupe jiwe hili la bahati, utakuwa tajiri.” Juma, kwa ujinga wake, akampa chupa zote tatu za maziwa ili apate lile jiwe. Akiwa amefurahi, alirudi nyumbani na kusema, “Mama tazama, nimepata jiwe la bahati! Hatuhitaji kuuza maziwa tena!”

Mama yake alihisi huzuni na hasira. Akamwambia, “Juma, dunia haitembei kwa ujinga. Akili ni mali kuliko mawe ya barabarani.”

Kutoka siku hiyo, mama yake alianza kumfundisha Juma kuhusu maisha, umuhimu wa bidii, na matumizi ya akili. Polepole, Juma alianza kubadilika. Akawa mwerevu, na akaacha kuwa mjinga.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872

0/Post a Comment/Comments