TEMBO ALIYECHEKA SANA

 

Na, Emakulata Msafiri

Kulikuwa na tembo mdogo aitwaye Toto ambaye aliishi kwenye msitu mkubwa wa kijani. Toto alikuwa tofauti na tembo wengine kwa sababu alipenda kucheka sana. Kila kitu kilimfurahisha—ndege akiimba, majani yakicheza na upepo, hata chura akiruka vibaya!

Siku moja, wanyama waliamua kufanya shindano la kuchekesha. Aliyecheka zaidi ndiye angepewa taji la "Mfalme wa Furaha." Tembo mdogo alijipanga vizuri katika mashindano hayo

Simba alitoa sauti ya kuchekesha, tumbili akacheza dansi ya ajabu, na paka mwitu akajaribu kuimba kama jogoo. Lakini hakuna aliyeweza kuwachekesha wanyama wote kama Toto.

Toto aliposimama, hakusema chochote. Alitazama tu paka mwitu aliyekuwa amevalia majani kichwani kama kofia, halafu... AKACHEKA! Na kicheko chake kilikuwa cha ajabu sana, kilienea kote msituni na kuwafanya wanyama wote wacheke bila kujizuia.

Na akapata zawadi ya taji la mfalme wa furaha katika msitu huo na wote walimpenda tembo mdogo kwa tabia yake ya kucheka kwasababu alikua anafurahisha wengi.

Hadi hata simba akaanguka chini akicheka!

Toto akapewa taji, na tangu siku hiyo, msitu ukawa mahali pa furaha kila wakati alipocheka.





emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments