Na, Emakulata Msafiri
Palikuwa na sungura mdogo aitwaye Tamu. Tamu alikuwa mwepesi wa miguu, mcheshi, lakini mara nyingi alikuwa mchoyo. Hakupenda kushirikiana na wanyama wenzake, hasa alipokuwa na chakula kizuri.
Siku moja, mvua kubwa ilinyesha, na sungura alipata mahindi mengi sana yaliyoanguka kutoka kwa gunia la mkulima. Akakusanya na kuyaficha kwenye pango lake. Ndama, rafiki yake, alifika akamuuliza:
"Tamu, unaweza kunipa mahindi kidogo tu? Sina chakula nyumbani."
Sungura akasema kwa kejeli na majivuno kiasi kwamba Ndama alishangaa sana
"Samahani, sina ya ziada. Haya ni kwa ajili yangu tu. Na ninaomba utoke nyumbani kwangu haraka sana nisikuitie mwizi sasa hivi".
Ndama alihuzunika lakini hakulalamika. Badala yake, aliamua kuendelea kutafuta chakula mwenyewe. Siku chache baadaye, mvua kubwa zaidi ilikuja na mafuriko yakasomba pango la sungura pamoja na mahindi yake yote.
Sungura alihangaika bila pa kwenda.Akaazimia kwenda kwa rafiki yake Ndama kwa mshangao wake, Ndama alimkaribisha nyumbani kwake na kumgawia chakula alichokikusanya.
Sungura akajifunza somo kubwa: "Kuwa mkarimu na kushirikiana ni muhimu, maana leo ni mwenzako, kesho unaweza kuwa wewe."Tangu siku hiyo, Tamu alibadilika na kuwa mnyama mwenye moyo wa upendo na mshikamano.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903873
Post a Comment