SUNGURA NA KOBE

 

Na, Emakulata Msafiri

Siku moja, sungura alikutana na kobe msituni. Sungura alikuwa mjanja

mwenye mbio sana. Akamcheka kobe kwa kuwa alikuwa akitembea polepole sana.

Sungura akasema kwa dharau, “Wewe ni mvivu kweli! Mimi ningeweza kukupita mara mia kwa dakika moja tu!”

Kobe akatulia na kumjibu kwa upole, “Sawa, basi twende mbio. Tuone nani atashinda.”

Mbio zikapangwa. Wanyama wote wakakusanyika kushuhudia. Sungura akaanza kukimbia kwa kasi sana, lakini alipofika katikati ya njia, akasema: “Nitapumzika kidogo, bado niko mbele sana.”

Akalala chini ya mti. Wakati huo, kobe aliendelea kutembea polepole lakini bila kusimama. Hatimaye, alipomkaribia sungura, akamkuta amelala fofofo. Akaendelea mbele na kufika mwisho wa mbio.

Sungura alipoamka, alikimbia kwa haraka lakini akakuta kobe tayari ameshashinda mbio!

Usimdharau mtu kwa mwonekano wake. Subira na bidii huleta ushindi.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments