Siku moja, sungura na kobe walikutana msituni. Sungura alijivuna kwa kasi yake ya kukimbia. Akamwambia kobe,
“Mimi ni mnyama mwenye kasi kuliko wote! Wewe ni wa polepole mno.”
Kobe akatabasamu tu, akamwambia,
“Ni kweli mimi ni wa polepole, lakini bado naweza kushinda mbio tukishindana.”
Sungura akacheka sana, “Hii ni kejeli! Haya, twende tukashindane.”
Wakakubaliana kuanza mbio asubuhi ya siku inayofuata. Mbio zilipoanza, sungura alikimbia sana hadi akawa mbali sana mbele ya kobe. Alipofika mti mkubwa, akasema,“Kobe yuko mbali sana. Wacha nilale kidogo nipumzike.”
Lakini aliposinzia, kobe aliendelea kutembea polepole lakini bila kusimama. Mwishowe, kobe akamfikia sungura aliyekuwa bado amelala, akampita polepole, na kufika mwisho wa mbio.
Sungura alipoamka, alikimbia kwa kasi lakini alipofika mwisho, alikuta kobe tayari ameshafika na kushinda.Pole pole huenda mbali. Usimdharau mtu kwa sababu ya mwonekano au kasi yake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment