MTOTO NI TUMAINI LA KESHO

Na, Emakulata Msafiri

Mtoto ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu na ni msingi wa jamii yoyote. Kupitia watoto, dunia huendelea kuwepo na kizazi kipya huandaliwa kwa ajili ya maisha ya baadaye. Mtoto huja duniani akiwa hana hatia, akiwa mweupe kama karatasi, na jamii ina jukumu la kumjaza maarifa, maadili na upendo.

Watoto wana tabia ya udadisi, kupenda kujifunza, kucheza na kuwa karibu na wale wanaowapenda. Kupitia michezo, mazungumzo na elimu, watoto hujifunza namna ya kuishi, kushirikiana na kuheshimu wengine. Ndani yao kuna ndoto kubwa, vipaji vya kipekee na ari ya kuleta mabadiliko makubwa.

Haki za mtoto ni pamoja na kupata elimu bora, huduma za afya, chakula, malazi, na ulinzi dhidi ya unyanyasaji na dhuluma. Ni jukumu la wazazi, walimu, jamii na serikali kuhakikisha watoto wote wanalelewa katika mazingira salama.

Pia, mtoto anahitaji kupewa nafasi ya kusema mawazo yake, kushirikishwa katika maamuzi yanayomhusu, na kuthaminiwa kama sehemu muhimu ya jamii. Mtoto anayepata malezi bora, elimu na upendo, hukua na kuwa mtu mzima mwenye mchango chanya katika jamii.

Kwa hiyo, kumtunza mtoto ni kuijenga jamii ya kesho. Kila mtoto ni lulu ya thamani na anapaswa kupewa fursa ya kung’ara katika maisha.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments