MALIPO YA UVIVU

 

Na, Emakulata Msafiri

Kulikuwa na mtoto mmoja aitwaye Juma, aliyekuwa akiishi kijijini na wazazi wake. Juma alikuwa mvivu kupita kiasi. Alikuwa hapendi kwenda shamba, kusoma wala hata kusaidia kazi ndogondogo nyumbani. Wazazi wake walimkanya sana, lakini hakubadilika.

Siku moja, baba yake alimwambia, “Juma, uende shambani ukalime mahindi leo. Ukifanya vizuri, nitakunulia kiatu kipya.” Lakini Juma alipiga miayo na kusema, “Acha tu, nitafanya kesho.”


Kesho ilipofika, mvua kubwa ilinyesha na kuharibu sehemu ya shamba ambalo lilikuwa halijalimwa. Jirani yao, Asha, ambaye kila siku alijitahidi kufanya kazi, alikuwa tayari amelima na kupanda mbegu zake mapema. Baada ya miezi michache, Asha alikuwa na mazao mengi ya kuuza na kula, lakini Juma na familia yake walikosa chakula cha kutosha.

Juma alianza kujuta, akatambua kuwa uvivu wake ulikuwa umewaumiza hata wazazi wake. Tangu siku hiyo, akaamua kubadilika. Alianza kuamka mapema, kusaidia shambani, na hata kujiunga na darasa la usiku kusoma.


Watu wa kijiji walishangaa kuona mabadiliko yake, na baba yake alipomwona akijitahidi, alimnunulia kiatu alichoahidi zamani—lakini safari hii, kama zawadi ya bidii.

Uvivu huleta hasara, lakini bidii huleta mafanikio makubwa inabidi Kila mmoja ajitume kwa lengo la kuleta mafanikio katika maisha.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments