Ña, Emakulata Msafiri
Katika msimu wa jua kali sana, mito na vijito vilikauka. Wanyama wengi walihangaika sana kutafuta maji. Miongoni mwao alikuwa ni Kunguru mweusi aliyeishi peke yake juu ya mti mkubwa kandokando ya kijiji.
Siku moja, baada ya kuruka kilomita nyingi bila mafanikio, Kunguru alichoka sana na kiu ilimzidia. Aliketi juu ya tawi na kusema kwa sauti,
"Ah! Laiti ningepata tone moja tu la maji!"Wakati huo huo, aliinua macho na kuona mwanga uking'aa kutoka kwenye kichaka. Kwa haraka akapaa kuelekea upande huo, na kwa mshangao wake, aliona kibuyu kidogo cha udongo kilichokuwa kimeachwa kando ya njia na wanakijiji.
Alipotazama ndani, aliona maji lakini yalikuwa chini sana, nje ya uwezo wake wa kuyafikia kwa mdomo wake mfupi. Kunguru alijaribu kuingia kichwa chake lakini alikaribia kuanguka. Alijaribu kulisukuma kibuyu lakini lilikuwa zito. Aliketi tena juu ya jiwe na kufikiria.
Ghafla, alisikia sauti nyuma yake."Shida gani rafiki yangu?" aliuliza Panya mdogo aliyekuwa akipita. Kunguru akasema, "Nina kiu sana lakini siwezi kufikia maji haya."
Panya alifikiria kisha akasema, "Tumia mawe! Weka mawe ndani, maji yatapanda." Kunguru alipata moyo na akaanza kutafuta mawe madogo. Kwa msaada wa Panya, waliokota mawe mengi na kuyaweka kwenye kibuyu. Kidogo kidogo maji yalianza kupanda.
Wakati huo, Kobe mzee naye alifika. Aliketi karibu na kibuyu, akasema, "Hamjui kuwa ni busara zaidi kutafuta njia ya pamoja ya kusuluhisha matatizo? Huu ndio mfano bora wa ushirikiano!"
Mwishowe, maji yalipofika karibu na mdomo wa kibuyu, Kunguru alikunywa. Alimpa Panya pia nafasi ya kunywa kwa kutumia kijiti kidogo, na hata Kobe alijilamba kidogo kwenye midomo, akafurahia. Wote walicheka, wakaahidi kusaidiana tena siku zijazo.
Akili ni muhimu, lakini ushirikiano huleta mafanikio makubwa zaidi.Tusiwe na haraka ya kukata tamaa – tukitumia akili na kuvumiliana, tutashinda matatizo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment